UZINDUZI wa
michuano ya Kombe la FA 2016 zitafanyika Tanga Novemba 19 katika Uwanja wa CCM
Mkwakwani kwa mchezo kati ya Muheza United dhidi ya Sifa Politan ya Temeke.
Msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 84 ambapo mabingwa wa mikoa pia watashiriki tofauti na mwaka jana ambapo timu 64 pekee kabla ya Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Azam mabao 3-1.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alisema bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 84 ambapo mabingwa wa mikoa pia watashiriki tofauti na mwaka jana ambapo timu 64 pekee kabla ya Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Azam mabao 3-1.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alisema bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
"Ligi
itazinduliwa Novemba 19 kule Mkwakwani Tanga kati ya Muheza United na Sifa
Politan na mwaka huu timu zimeongezeka tofauti na mwaka jana ambapo tunatarajia
ushindani mkubwa," alisema Lucas.
Pia Lucas
alisema michuano hiyo itaonyeshwa moja kwa moja (mubashara) na kituo cha
Luninga cha Azam TV ambao ndiyo wadhamini wakuu kwa miaka mitano kutokana na
mkataba ulioingiwa na TFF.
Lucas alisema matarajio ya Shirikisho kuona ligi yenye ushindani baada ya timu kuongezeka kulinganisha na mwaka uliopita.
Lucas alisema matarajio ya Shirikisho kuona ligi yenye ushindani baada ya timu kuongezeka kulinganisha na mwaka uliopita.
Mwaka huu
kuna timu 16 za Ligi Kuu Tanzania Bara, timu zote 24 za Ligi Daraja la Kwanza
(FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL) na timu 22 za mabingwa wa mikoa na
yatakuwa ya mtoani na yataendeshwa kwa raundi tisa.
Raundi ya kwanza
itashirikisha timu 22 za Mabingwa wa
Mikoa katika makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu
zitaingia raundi ya pili.
Raundi
ya pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya kwanza na
kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya timu zote kuwa 32
kwa hatua ya pili.
Raundi ya tatu
itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane
zitakazoingia hatua ya nne.
Raundi
ya nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha timu nane
zilizoshinda raundi ya tatu kufanya timu zote kuwa 32.
Raundi ya tano,
itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya nne na kumuisha timu zote 16
zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya timu zote katika
raundi hii kuwa 32.
Raundi ya sita
itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika raundi ya tano na mzunguko huo
utaitwa Hatua ya 16 Bora.
Raundi
ya saba itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na mzunguko
huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .
Raundi ya nane
ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu raundi ya saba (Robo Fainali) na
mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni nusu fainali.
Raundi ya tisa
itashirikisha timu mbili zilizofuzu raundi ya nane na washindi hao wa nusu fainali
na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa msimu wa 2016/2017.
Tanzania mwakani
kwenye kpmbe la Shirikisho itawakilishwa na timu ya Azam FC baada ya kupoteza
kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga ambao watacheza ligi ya Mabingwa
Afrika.
No comments:
Post a Comment