SERIKALI imevitaka Vyama, Mashirikisho na klabu za
Michezo nchini kufuata taratibu na sheria zinazoendesha michezo na kuacha
kutumia vyombo vya habari kama mawakala.
Akizungumza
na wandishi wa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja,
alisema vyombo vyote vilivyo chini ya ofizi yake vinafahamu hatua mbalimbali za
kupitia katika kutatua tatizo au
changamoto kwakuwa zinaongozwa na katiba
“Naviagiza Vyama, mashirikisho na klabu kufuata
taratibu na sheria zinazowaongoza katika kuendesha michezo na kutatua matatizo
yao na kwa kuzingatia miongozo ili kuleta maendeleo ya michezo nchini badala ya
kuwatumia Wanahabari katika kutafuta ufumbuzi wa mambo yao” alisisitiza
Kiganja.
Pia Kiganja alisema hasara za kutumia vyombo vya
habari kunadi migogoro kunasababisha wadhamini kukata tamaa kusaidia sekta ya
michezo na kuongeza kuwa serikali badala ya kushughulikia maendeleo ya michezo,
inageuka mahakama au wasikiliza migogoro kwani mwenendo wa michezo inapata
taswira mbovu kwa ajili ya watu wachache wenye uroho na tamaa za madaraka
Kiganja alisema baraza linavitaka vyama vya michezo
nchini kujifanyia tathmini kama usajili wao unafanana na kazi wanazoziratibu
kulingana na matakwa ya usajili wao.
Kiganja alieleza kuwa, serikali imeajiri maafisa
mchezo mikoa yote, hivyo wawasiliane nao ili vyama hivi vishuke huko Mikoani,
Wilayani hadi kwenye kata ambako ndiko wanamichezo wengi walipo na kuache
kung’ang’ania kukaa na kufanya kazi Dar es salaam.
“Miaka ya
1980-90 Tanzania ilikuwa inaongoza katika michezo mingi ndani ya Afrika Mashariki,
lakini leo hii tunanunua wachezaji kutoka Burundi, Rwanda, Kenya, na Uganda,
hivi tatizo letu Tanzania ni nini” ? aliuliza Kiganja.
No comments:
Post a Comment