Mtihani huo
ambao ni maalumu kwa ajili ya msimu mpya wa kupewa beji mpya na msimu mpya wa
Ligi Kuu Tanzania Bara ulianza juzi na unatarajiwa kumalizika kesho.
Waamuzi
waliofeli ni John Kanyenye, Waziri Sheha, Kudra Omar, Grace Wamara huku Sophia
Mtongori yeye hakufika kwenye mtihani huo.
Kozi hii
ambayo inaendeshwa na wakufunzi wa kimataifa Carlos Henrique, Mark Mzengo na
Felix Tangawarima ilikuwa na waamuzi 30
huku 18 ni wale wenye beji na 12 ni watarajiwa (elite)
Waamuzi hao
waliripoti Julai 24 na juzi waliingia kwenye mtihani wa utimamu mwili na
kuanzia jana wanaendelea na kudurusu marekebisho ya sheria 17 za soka ambalo
zimefanyiwa marekebisho.
Gazeti hili
lilishuhudia waamuzi hao wakitafsiri kwa vitendo sheria huku wakisimamiwa na
wakufunzi wao.
No comments:
Post a Comment