KIPA wa
Mbeya City, Juma Kaseja ameteuliwa kuwa kocha wa makipa wa timu ya Vijana ya
soka walio chini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’
alisema kuwa Kaseja anachukua nafasi ya kocha Mharami Mohamed ambaye atakuwa
kwenye kozi ya juu ya makipa.
“Serengeti
boys imeondoka leo kwenda kuweka kambi nchini Madagascar kwa ajili ya
kujiandaa na mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini na Kaseja
atakuwepo kwenye kocha benchi kwenye mchezo huo”, alisema Lucas.
Pia Lucas
alisema kwenye kikosi hicho atakosekana pia kocha msaidizi Seba Nkoma ambaye
yupo kwenye kozi ya makocha ya leseni A.
Serengeti
boys itaweka kambi Madagascar kwa siku kumi kabla ya kuikabili Afrika Kusini
Agosti 6 na watarudiana Agosti 21 hapa nyumbani.
Endapo
Serengeti boys itafanikiwa kuitoa Afrika Kusini itapambana na timu kati ya
Namibia au Congo Brazaville na ikiwa itafanikiwa kushinda itakuwa imefuzu
kwenda Madagascar.
No comments:
Post a Comment