Real Madrid hoi!! wamelala kwao Bernabeu!Vichwa chini!!Kipa
wa Juventus akishangilia Timu yake kutinga Fainali itakayochezwa mwezi
ujao juni tarehe 06,2015 Olympiastadion, Berlin, GermanyKipindi
cha pil dakika ya 57 Álvaro Morata aliwasawazishia bao Juventus na
kufanya 1-1 na kuwaweka katika Hali ngumu Real Madrid. Sare hii inawapa
Ushindi Juventus kupitia bao lake mchezaji wa Zamani wa Real Madrid
Alvaro Morata kipindi cha pili na kwa kuwa Juve walikuwa wako mbele
katika mechi ya kwanza walipotoka bao 2-1 na hivyo kufanya Jumla kuu Agg
kuwa 2-3 hivyo Juve kwenda Fainali. Fainali sasa kuchezwa Mwezi wa Sita
(June) tarehe 06, 2015 kati ya Juventus na Barcelona.Pia
Fainali hiyo mpenzi wa bukobasports.com itakuwa ya aina yake kwani Luis
Suarez kukutana uso kwa uso na Evra na Chiellini waliomfanya afungiwe
Jumla ya Mechi 17 na Miezi Minne, na kutwangwa Faini ya Jumla ya Pauni
Elfu 40 kipindi hicho.Hatari tupu!! Ronaldo hakulemba kabisa kupiga penati leo hii!Cristiano Ronaldo akshangilia bao lake la PenatiDakika
ya 23 kipindi cha kwanza Cristiano Ronaldo anaipachikia bao la kwanza
Real Madrid kwa mkwaju wa Penati na kufanya 1-0 dhidi ya Juventus. Bao
hilo la Cristiano Ronaldo lilidumu na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele
na huku jumla ya magoli ya mtanange wa kwanza na huu japo bado dakika
ya 45 ikiwa ni (Agg 2-2).Ronaldo akishangilia bao lake mbele ya Mashabiki wao Ndani ya Uwanja wa BernabeuWachezaji wa Juve wakimjia juu Mwamuzi wa mtanange baada ya kutokea penatiRonaldo chini akiutafuta mpira!
VIKOSI:
Real Madrid wanaoanza: Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Rodriguez, Isco, Kroos, Bale, Benzema, Ronaldo
Real Madrid Akiba: Navas, Pepe, Fabio Coentrao, Hernandez, Arbeloa, Jese, Illarramendi
Juventus wanaoanza: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Pogba, Vidal, Tevez, Morata
Juventus akiba: Storari, Coman, Llorente, Barzagli, Padoin, Sturaro, Pereyra

No comments:
Post a Comment