Hadi sasa upo uhakika mkubwa wa England kuwakilishwa kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na Mabingwa Chelsea, Timu ya Pili Man City, Timu ya 3 Arsenal na Timu ya 4 Man United.
WAkati Chelsea tayari wameshaichukua Nambari Wani, Mshindi wa Pili hadi wa 4 wa Ligi bado hajathibitika ingawa Man City na Arsenal zina uhakika mkubwa wa kutwaa Nafasi za Pili na za Tatu ukulinganisha na Man United kutokana na wingi wao wa Pointi.
Man United ndio walioshinda huko Emirates 2-1 katika Mechi ya kwanza kati yao ya Ligi Msimu huu.
No comments:
Post a Comment