Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 16, 2015

TFF YAKANA TAARIFA YA BUNDALA


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limesema taarifa iliyoandikwa na Gazeti moja la tarehe 15, Mei 2015 yenye kichwa cha habari “Nkurunziza ameweka picha mbaya katika soka” haina uhusiano na TFF.

Katika taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael Bundala amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa nchini Burundi.

TFF imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli hii ni mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF unafuatilia  ili kujua ni hatua gani zichukuliwe.

Jukumu la TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si vinginevyo. 

TFF inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na baraka katika nchi yao.

No comments:

Post a Comment