NA Mwandishi Wetu,Tanga.
MKUTANO Mkuu wa Dharura wa Wanachama wa Klabu ya Coastal Union unatarajiwa kufanyika kesho Mei 17 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.
Sababu za Mkutano huo kufanyika katika Ukumbi la Polisi Mesi ni kutokana na makao makuu ya klabu ya Coastal Union kuendelea mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa na upigaji picha wananchi
kwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na unafanyika kufuatia vikao vya maridhiano ya Uhakikiwa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.
Ambapo alisema baada ya kumalizika vikao hivyo,Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment