Mshambuliaji huyu ameelekea nchi Marekani kwenda kuonana na madaktari Peter Asnis ili kujua kama anahitaji kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo lake.
Majeruhi yamekua yakimuandama mshambuliaji huyu katika msimu huu na kushindwa kuonyesha cheche zake za kuzifumania nyavu.
Aliumia mguu mwezi September wakati wa michezo ya kimataifa na kabla ya kuumia misuli akiwa mazoezini.
Sturridge alijiunga na Liverpool kwa usajili wa kiasi cha pauni milioni 12 mwezi January mwaka 2013 na amefunga mabao 24 katika michezo yote aliyoichezea timu hiyo.
No comments:
Post a Comment