BONDIA Francis Cheka anatarajia kupanda ulingoni kwa mara
ya kwanza baada ya kutoka jela Mei 30 kupambana na bondia Kiatchai Singwancha
kutokaThailand.
Pambano hilo litakuwa la raundi kumi na utachezwa kwenye
Ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia pambano hilo promota Kaike Siraju amesema
kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa na mabondia wa
utangulizi wote wanatarajia kusainishwa mkataba wa kupanda ulingoni wiki hii.
“Tumeandaa pambano hili kwa ajili ya kumkarisha ndugu
yetu Cheka ambaye anatumikia kifungo cha nje baada kupatikana na hatia ya
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kumpiga meneja wa baa”,
alisema Siraju
Pambano litasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini
P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa
Siraju amesema kuwa bondia wa Thailand atawasili nchini
siku tatu kabla ya pambano hivyo kuwatakamashabiki kwenda kumwona kipenzi chao
Cheka akiwa furaha baada ya kimya kirefu
No comments:
Post a Comment