Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 30, 2015

SAMATA ALIVYOIOKOA TAIFA STARS KULALA KWA MALAWI KIRUMBA


Taswira Viongozi na Timu zote mbili wakati wa dakika chache kumbuka Kiongozi wa mpira Aliyetangulia mbele ya haki kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Star Sylvester Marsh aliyefariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Mjini  Mwanza.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika Mpambano huo wa Taifa Stars na Malawi CCM Kirumba  Jijini Mwanza leo Jumapili tarehe 28.03.2015
Wimbo wa Taifa uliimbwa kabla ya Mechi kuanza, (Picha na Faustine Ruta)

Timu zote mbili kwenye mstari tayari kwa kuanza kipute

Kikosi cha Malawi baada Wimbo wao wa Taifa kumalizika kuimbwa

Kikosi cha Taifa Stars kikiimba wimbo wa Taifa
Viongozi wakisalimia Mashabiki walioingia kwa Wingi Uwanjani hapo CCM Kirumba, Picha na Faustne Ruta
Timu zikisalimiana

Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza

Waamuzi wa Mtanage

Kikosi cha Malawi

Tayari kwa mpambano kuanza..

Shilingi kutafuta uelekeo
Picha ya PamojaBao 1-0 dakika ya tatu tu Malawi walipata bao kupitia kwa Esau Kanyenda baada ya mapeki wa Stars kujichanganya
Wachezaji wa Malawi wakipongezana baada ya kupata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Esau Kanyenda kwa kufanya 1-0

Mchezaji wa Malawi akimiliki mpiraShomari Kapombe akifanya yake

Taifa Stars 0-1 Malawi dakika ya 3 mapema Malawi walishachafua ubao

Kipa wa Malawi akiondosha mpira langoni mwake


Pisha!

Fundi!

Kipa wa Malawi akiondosha mpira kwa kuupangua kutoka eneo la hatari

 Mashabiki jukwaa kuu

Meza Kuu Rais wa Tff  Bw. Jamal Malinzi nae alikuwepo kushuhudia kipute!
Nyomi
Katikati ni Bw. Abdrazack kutoka Mjini Bukoba/Kasibante 88.5 FM Radio akitangaza live mpira huo kutoka CCM Kirumba Jijini Mwanza
Mashabiki waliingia kwa wingi

Mbwana Samata mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea TP Mazembe ya Congo ameisaidia Timu ya Taifa ya Tanzania isiaibike Nyumbani baada ya kusawazisha bao katika mechi ya kimataifa ya Soka kati ya Taifa Stars na Malawi.
Pambano hilo lililopigwa katika Jiji la Mwanza uwanja wa CCM Kirumba lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Stars wakitawala kwa kipindi kirefu bila ya mafanikio.
Goli la Malawi likifungwa dakika ya 3 na Esau Kanyenda mchezaji anayekipiga katika klabu ya Plolokwane City ya Afrika Kusini baada ya kipa wa Stars Mwadini Ali kushindwa kuudaka mpira wa kona huku Mabeki wakishindwa pia kumzuia mfungaji kupiga mpira ulioandika bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.


Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha wa Taifa Stars Mrisho Ngasa aliyeingia kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo na Salum Abubakari kuchukua nafasi ya Kiemba yaliisaidia Taifa Stars kupata goli la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Mbwana Samata akiitumia vizuri pasi ya Mrisho Ngasa.
Licha ya kupiga mashuti 10 ambayo matano yalilenga goli Stars hawakufanikiwa kuongeza bao na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.



Mpaka mapumziko Stars ilikuwa nyuma ya 1-0

Waamuzi wakitoka kwenda kupumzika wakati wa mapumziko dakika chache

Kipindi cha pili tunafanyaje??? Ngassa aingie au??

Muuaji wa bao la Malawi Essau Kanyenda wakati wa mapumziko

Yale yale Ngassa na wenzake wakitoka Uwanjani kwenda kujumuika na kusikia neno kutoka kwa kocha mkuu Mart Nooij nini kinafanyika kipindi cha pili.

Patashika kwenye lango la Malawi kipindi cha pili. Hadi mapumziko Malawi walikuwa mbele kwa goli 1-0, na kupelekea Stars kurejea kipndi cha pili kwa nguvu, huku kukifanyika mabadiliko ya kumtoa Amri Kiemba na Haruna Chanongo na nafasi zao kuchukuliwa na Salum Aboubakari na Mrisho Ngassa.

Mbwana Ally Samatta akishangilia bao baada ya kuisawazishia bao Taifa Stars kwa kufanya 1-1 dakika ya 76 kipindi cha pili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo hii, Picha na Faustine Ruta

Asante baba!! Samatta akipongezwa na Ulimwengu

Shabiki akifanya mbwembwe zake baada ya Taifa Stars kusawazisha bao1-1

Samatta akipongezwa na Ulimwengu

Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars nao walimpongeza Samatta

Wakirudi kati kuanzisha mpira


Pongezi kwa Samatta Ally Mbwana


Mtanange umemalizika dakika 90 kwa nguvu sawa 1-1

Waandishi wa Habari wakipata mahojiano moja kwa moja kutoka kwa Afisa habari wao Malawi akiwa sambamba na Baraka Kizuguto wa Tanzania kupitia Tff
Taifa stars: Mwadin Ally, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Aggrey Morise, Erasto Nyoni, Amri Kiemba/Salum Aboubakari, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu/John Bocco, Mbwana Samata na Haruna Chanongo/Mrisho Ngassa

No comments:

Post a Comment