UONGOZI wa Mzizima Motorsports Club (MMSC) umeandaa
mashindano ya mbio za magari yatakayofanyika Aprili 12 mjini Bagamoyo, Pwani.
Akizungumza jijini Katibu Mkuu wa Mzizima Motorsports Club,
Hidaya Kambanga alisema kuwa mashindano
hayo yatakuwa ya umbali wa kilometa moja na yatahusisha waendasha,
baiskeli, pikipiki na magari.
“Mashindano haya yatakuwa yanahusisha waendasha baiskeli,
pikipiki na magari ya aina zote kwenye umbali wa kilometa moja lengo likiwa ni
kuhamasisha madereva mbio za magari badala ya kukimbizana barabarani kwani
usalama unakuwa mdogo”, alisema Hidaya.
Pia alisema madareva watakaopenda kushiriki wanatakiwa
kulipa ada ya 20,000 na wadereva ambao wanaruhusiwa ni wale wenye umri wa miaka
19 na kuendelea.
Hidaya alisema zaidi ya madereva 150 wanatarajiwa kushiriki
na kuwaomba wengine ambao wanapenda kushiriki kujisajili na kulipa ada.
Naye Mshauri wa mambo ya ufundi wa Mzizima, Athman Hamisi
alisema madereva wote wanatakiwa kuja na kofia ngumu (element), kizima moto
(fire extinguisher) na akasisitiza kabla ya kuwasha gari kuanza mbio
watahakikisha kila dereva amefunga mkanda kw ajili ya usalama.
Pia alisema dereva ambaye atakuja akiwa amekunywa kilevi
chochote ataruhusiwa kuingia kwenye mashindano.
Mashindano hayo ya Mbio yamedhaminiwa na Redbull, Majipoa,
grassroots sports and events na National Rally Company (NRC)
No comments:
Post a Comment