Beno njovu katibu wa Yanga akitoa ufafanuzi ya uteuzi wa kamati mpya |
Yusufu Manji (kushoto) na Clement Sanga kulia wana nguvu ya wanachama ya mkutano wa Januari 20 2013 kufanya uteuzi hata kabla ya katiba kuidhinishwa |
KLABU
ya Yanga imelazimika kutoa ufafanuzi juu ya uteuzi mpya wa wajumbe wa
kamati ya utendaji mpya ulifanywa na mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu
Manji na makamu wake Clement Sanga ambayo itaanza kazi yake kuanzia
rasmi Agosti mosi.
Itakumbukwa
kuwa ni jana tu katibu wa klabu hiyo kongwe hapa nchini Beno Njovu
mbele ya waandishi wa habari alitangaza kuwa Mwenyekiti na Makamo
Mwenyekiti wa Klabu ya hiyo kwa mamlaka waliyopewa na Wanachama,
kubadilisha, kupunguza
au kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati
wowote, kulingana na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya
YANGA.
Viongozi hao katika taarifa yao hiyo walitangaza kuzivunja kamati zote ambazo ziko chini ya
Kamati ya Utendaji kuanzia tarehe 31 Julai, 2014.
Akiongea
na Rockersports Njovu amesema viongozi hao wamefanya mabadiliko hayo
kufuatia nguvu kubwa waliyopewa na wanachama katika mkutano wao mkuu wa
klabu hiyo uliofanyika Januari 20 2013 lakini pia ibara ya 28 ya katiba
mpya ya klabu hiyo ambayo bado haijaidhinishwa na shirikisho la soka
nchini TFF.
Amesema
ibara hiyo ya 28 inazungumzia juu ya muundo wa kamati ya utendaji na
namna kamati hiyo inavyopatikana na kwa kuwa uongozi huu umeshakuwa na
miezi mitatu yangu kupata ridhaa ya wanachama ya kuendelea kwa kipindi
kingine cha mwaka mmoja kulikuwa kuna haja ya kufanyika uteuzi mpya wa
wajumbe wa kamati mbalimbali ili kufanya kati ya klabu hiyo.
Njovu
amesema wajumbe walitoa ridhaa ya kuendelea na uongozi kwa mwenyekiti
na makamu wake tu, hivyo wasingeweza kufanya kazi za kiutendaji na
usimamizi wa shughuli za kila siku za klabu na sekretarieti iliyopo
pekee yake.
Wajumbe hao wapya ni Abubakar Rajabu(Miradi wa Jangwani City),Sam Mapande (Sheria na Utawala Bora),George Fumbuka (Uundwaji wa Shirika),Waziri Barnabas(Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano na Wafadhili),Abbas Tarimba(Mipango na Uratibu),Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed(Uendelezaji wa Mchezo),Musa Katabalo(mauzo ya Bidhaa)Mohammed Bhinda(Ustawishaji wa Matawi)David Ndeketela(Uongezaji wa Wanachama) na Mohammed Nyenge(Utangazaji wa Habari, Taarifa, Matangazo).
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ILIYOUNDWA UPYA WATASIMAMIA KIMSINGI KAMATI NDOGO ZIFUATAZO:
•Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam Mapande
•Kamati ya Uchumi na Fedha - Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri KLABUBarnabas
•Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Ufundi - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
No comments:
Post a Comment