Hali
ya Jeraha la mshambuliaji wa Barcelona Neymar kufuatia kugongwa kwa
nyuma wakati wa fainali ya kombe la dunia na kupelekea kufanyiwa
upasuaji wa mgongo sasa anaendelea vizuri ambapo amenza kula bata
taratibu kwa kutoka na mpenzi wake Bruna Marquezine fukweni nchini
Hispania.
Wapenzi
hao wamekuwa wakivinjari fukweni Formantera ambapo Neymar
amekamilikisha siku za kuendelea kutembea na kitu kilichokuwa kinampa
msaada wa mgongo (yaani Back-Support).
Neymar
hakucheza michezo miwili ya mwisho ya timu yake ya taifa katika
michuano ya kombe la dunia kufuatia kupata kuumia vibaya mgongoni katika
mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia.
Wakiwa wanabadilishana mawazo akiwa na washikaji zake. Neymar pamoja na Bruna Marquezine kwenye kiboti ambapo Neymar amevalia Back-Support
Holidays: Wapenzi wakiwa mapumzikono Formentera, nchini Hispania
Umaarufu ni shidaa: Neymar akisimamishwa na mashabiki ufukweni kwa lengo la kupata picha kwa pamoja
Neymar
anatarajiwa kuungana na mshambuliaji mpya wa Barcelona Luis Suarez huku
vyombo vya habari nchini Hispania vikiandika sana kuwa kwa pamoja
watatengeneza partnership kwa kushirikiana na Lionel Messi.
Neymar
alijiunga na Barcelona kiangazi iliyopita ambapo ameifungia magoli tisa
katika jumla ya michezo 26 aliyoichezea klabu hiyo katika ligi.
Neymar akijitahidi kutoka kwenye kiboti cha kukodi.
No comments:
Post a Comment