Bondia
Nasser Mafuru wa Tanzania amepoteza mchezo wake dhidi ya Jessie Lartey
wa Ghana uzito wa kilo 60 michezo ya Jumuiya ya Madola inayofanyika huko
Glassgow nchini Scotland, kufuatia kushindwa kupanda ulingoni kwa kile
kilichoelezwa kuwa alipatwa na maradhi ya tumbo ghafla.
Akiongea
na Rockersports kocha mzalendo wa mchezo huo John Mwakipesile amesema
Mafuru amepatwa na maswahibu hayo muda mfupi kabla ya kupanda ulingoni
wakati akipasha mwili joto na na ndipo akashikwa na tumbo la kuhara
kabla ya taarifa kupelekwa kwa wasimamizi wa mchezo huo ambao
waliumaliza mchezo huo nje ya ulingo.
Jana
akizungumza na mtandao wa Rockersports, Mafuru alisema amemuona
mpinzania wake kutoka Ghana Jessie Lartey na kwamba asingeweza kufua
dafu kufuatia maandalizi yake mazuri.
Hiyo
inakuwa ni karata ya pili kupotea kwa upande wa Tanzania kufuatia
bondia nahodha Selemani Kidunda usiku wa jana kupigwa na mpinzania wake
kutoka Nigeria Kehinde Ademuyiyiwa licha ya kuwa vizuri sana wakati wa
mchezo.
Usiku
huu bondia mwingine mtanzania Fabian Gaudence atapambana na Steven
Thanki wa malawi uzito wa kilo 64 kabla ya Ezra Paul kucheza dhidi ya
Bye kesho jioni uzito wa kilo 52 naye Mohamed Hakimu akimsubiri Sumit
Sangwan wa India jioni uzito wa kilo 81.
Kesho kutwa Emilian Patrick atacheza na Bashiri Nasir wa Uganda kilo 56 naye Hamed Furahisha atababiliana na Paddy Barnes wa Ireland Kaskazini kilo 49.
No comments:
Post a Comment