Wakati
wachezaji wa Arsenal wakijipanga kwa ajili ya kuelekea kwenye Emirates
Cup, Mesut Ozil bado anaendelea kula raha za mapunziko akiwa na demu
wake.
Ozil
mwenye umri wa miaka 25 alionekana akifanya yake akiwa na mpenzi wake
Mandy Capristo wakijipunzisha kwa bwawa la kuogelea la hoteli ya kitalii
mjini Las Vegas.
Bingwa
huyo wa kombe la dunia wa Ujerumani naye kama ilivyo kwa wachezaji
wengine wa Ujerumani ambao walipewa mapunziko marefu marefu na vilabu
vyao, pia imekuwa hivyo kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid
ambaye amepata ruhusa ya bosi wake Arsene Wenger na hatakuwepo kikosini
wakati wa kuanza msimu.
Arsene Wenger amesema Ozil hatakuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.
Mesut Ozil na mpenzi wake Mandy Capristo wakipumzika baada ya msimu mrefu na klabu yake pamoja na timu ya taifa.
Meneja mfaransa Wenger amekaririwa akisema
'Nimewapa mapumziko wote Ozil, Lukas Podolski na Per
Mertesacker mapunziko mazuri kwasababu wachezaji ambao hucheza fainali ya kombe la dunia wanahitaji wanahitaji mapumziko
Arsenal imeelekea Marekani kwa maandalizi ya msimu ambapo ilifungwa na timu ya Thierry Henry ya New York Red Bull bao 1-0.
Arsene
Wenger anamatumaini kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kiasi katika
michuano yao ya mwisho ya maandalizi ya msimu huko Landoni ya Kaskazini
ambapo watacheza dhidi ya Benfica mchana na baadaye dhidi ya Monaco siku
itakayo fuata.
No comments:
Post a Comment