Wakati
Barcelona ikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya na wakitarajia kucheza
mchezo dhidi ya Nice mwishoni mwa wiki, mlinzi wa kushoto Dani Alves
ameonekana akiota la ufukwe huko Marekani.
Mlinzi
huyo wa kushoto wa Barcelona na Brazil amekuwa akifurahua ufukwe wa
Miami na anatarajiwa kuchelewa kidogo kwenye mazoezi ya kuanza msimu
baada ya kombe la dunia kumalizika.
Kumekuwepo
na tetesi juu ya kuondoka kwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31
kiungani Catalanya licha ya mwenye kutanabaisha kuwa atacheza tena
katika klabu yake ya Barcelona msimu ujao.
Utamu wa jua: Mlinzi wa kushoto Alves yuko Florida akila raha wakati kikosi cha Barcelona kikiwa mazoezini England
Brazil:
Alves hakupata nafasi ya kuendelea na michezo miwili ya mwisho ya kombe
la dunia ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Maicon
Alves amekuwa katika tetesi za kuondoka Katalunya lakini mwenye anasema angependa kusalia hapo kama itawezekana.
No comments:
Post a Comment