Ni
ukweli ulio dhahiri kuwa mashabiki wengi wa soka huwa na kiu ya
kukutana na wachezaji wao wanaowapenda, lakini kwa binti mmoja
ilionekana imezidi kiwango pale alipokutana na uso kwa macho na Steven
Gerrard na kushindwa kujizuia kwa kulia kwa sauti na kububujikwa na
machozi pasi na kuzuizi wala aibu.
Nahodha
huyo wa Liverpool alikuwa akitia saini 'autographs' alipokutana na
mashabiki hao huko ziarani nchini Marekani baada ya kusimama na kutoa
nafasi ya kupiga picha kupitia simu za mashabiki wake yaani 'Selfie'
hapo ndipo tafrani ilipoanza pale msichana huyo alipofyatuka na jineno
zito mdomoni 'I
love you' na kuzozomoa kilio kilichofuatiwa na machozi ya kumwaga.
Gerrard
akaamua kuendelea na zoezi lake la kusaini 'autographs' za mashabiki
wengine lakini bado msichana huyo akaendelea kusisitiza anataka
kusainiwa pia kwenye simu nyingine yenye picha ya 'Steven Gerrard' kitu
ambacho hakufanikiwa.
Wenzake waliokuwa naye walianza kuona kama burdani ambapo walitabasamu na kuondoka naye.
KIungo
huyo mwenye umri wa miaka 34 ameweka historia ya kuwafanya mashabiki
wake kulia ambapo iliwahi kutokea pia katika ziara ya mwaka jana barani
Asia.
Ma-Selfie
na mashabiki: Hapa Gerrard ndipo alipozua kilio cha haja akipiga picha
na shabiki wake mdada aliyezua kilio cha mwaka baada ya kumuona shujaa
wake kiasi kumfanya kushinda kufurahia wasaa huo
Simu yangu yenye picha yako: Nahodha wa Liverpool asini picha yake nyuma ya simu.
Princeton: Gerrard na wachezaji wa Liverpool walikuwa wakifanya mazoezi kabla ya mchezo dhidi ya Manchester City
Du! Michozi ya kumwaga: Huyu dada alikuwa anyamaziki licha ya kubembelezwa baada ya tukio
Steven Gerrard anaendelea kukutana na mashabiki wake Princeton University ambao walikuwa wakitaka zaidi autograph
No comments:
Post a Comment