Chika Amahala akutwa na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu |
Mshindi wa medali ya dhahabu toka Nigeria Chika
Amalaha amesimamishwa kwa muda kushiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya
Madola baada ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alishinda
medali ya dhahabu katika kunyanyua vitu vizito baada ya kuinua uzito wa
jumla ya kilo 196, kwa upande wa wanawake wenye uzito wa kilo 53.
Medali hii ni sawa na bure |
Vipimo vya awali alivyofanyiwa
vilionyesha kuwa ametumia dawa aina ya Amilorde na hydrochlorothiazide
,ambazo zote zimepigwa Marufuku michezoni.
Binti huyo anatarajiwa kuchukuliwa kipimo cha pili leo.
Mwanariadha huyo chipukizi wa Nigeria alishinda
medali ya dhahabu Ijumaa iliyopita huku Dika Toua akiipatia Papua New
Guinea medali ya ya kwanza kwenye michezo hii ya Jumuiya ya madola mwaka
huu inayoendelea mjini Glasgow,ambapo Santoshi Matsa wa India aliipatia
medali ya Shaba nchi yake kwea kushika nafasi ya tatu.
Amalala ni mwanariadha wa kwanza kugundulika
kutumia dawa za kuongeza nguvu kwenye michezo hiyo ya jumuiya
madola,ambapo Mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi mita 400 Rhys
Williams kutoka Wales,na mkimbiaji wa mbio za Mita 800 Gareth Warburton
pia wa Wales wakiwa wamelazimika kukosa michuano hiyo kutokana na
kukabiliwa na tuhuma za matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Wanariadha wote hao wanakanusha kutumia dawa yoyote iliyopigwa marufuku huku wakiwa wanafahamu
No comments:
Post a Comment