Divock Origi hatimaye akamilisha uhamisho wa kujiunga na Liverpool |
Hatimaye
Liverpool imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Belgium Divock Origi
akitokea klabu ya Lille ya Ufaransa kwa kitita cha pauni milioni £10.
Origi atasalia Lille mpaka 2015 |
Origi
mwenye umri wa miaka 19 kimsingi amekubali kuingia kandarasi ya miaka
mitano lakini ataendelea kusalia katika klabu yake hiyo kwa mkopo msimu
ujao huku akitarajiwa Anfield
mwakani 2015.
"Ninafuraha na kujisikia fahari kujiunga na klabu kubwa kama Liverpool nimefurahi sana"
Origi alicheza michezo yote mitano ya Belgium katika kombe la dunia
la FIFA 2014 kuelekea robo fainali na laifanikiwa kufunga goli katika
mchezo dhidi ya Urusi
Wachezaji waliosajiliwa na Liverpool uhamisho huu wa kiangazi ni hawa wafuatao
Mshambuliaji Rickie Lambert miaka 32, amesaini kwa pauni milioni £4 akitokea Southampton
Kiungo Adam Lallana miaka 25, amesaini kwa pauni milioni £25 akitokea pia Southampton |
Kiungo Emre Can, miaka 20, amesaini kwa pauni milioni £10 akitokea Bayer Leverkusen |
Winga Lazar Markovic, miaka 20, amesaini kwa pauni milioni £20 akitokea Benfica |
Mlinzi Dejan Lovren, miaka 25, amesaini kwa pauni milioni £20 Southampton |
Na sasa mshambuliaji kinda Divock Origi, mwenye umri wa miaka 19 amesaini kwa pauni milioni £10 akitokea Lille |
Origi alianza soka lake katika klabu ya Genk kabla ya kuelekea Lille akiwa ana umri wa miaka 15.
No comments:
Post a Comment