Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 9, 2014

WAYNE ROONEY, "NITAKOMAA UNITED MPAKA NIVUNJ REKODI YA SIR BOBBY CHARLTON" MPAKA SASA CHARLTON ANA 249, ROONEY 208.

Wayne Rooney amedokeza kuwa atasaini Mktaba mpya na Klabu yake Manchester United.
Wiki iliyopita kulivuja habari kuwa Rooney yuko tayari kusaini Mkataba mpya kuendeleza huu wa sasa unaomalizika mwishoni mwa Msimu ujao na ambao utakuwa ukimlipa Pauni 300,000 kwa Wiki.
Jana Rooney alitamka kuwa anategemea kuivunja Rekodi ya Ufungaji Magoli ya Manchester United iliyowekwa na Lejendari Sir Bobby Charlton nah ii ilileta uthibitisho kuwa atasaini Mkataba mpya.

Rooney alisema: “Siku zote nimesema mie natilia mkazo Soka langu tu na kujaribu kufanya vyema ili Timu iwe na mafanikio!”
Hadi sasa Sir Bobby Charlton ndie Mfungaji Bora wa Man United akiwa na Bao 249 na Rooney amefikisha Bao 208.
Akizungumzia Rekodi hiyo, Rooney alisema: “Kama nitaifikia, nitasikia fahari kubwa kwa sababu ipo kwa muda mrefu!”
Pia zipo fununu kuwa Rooney ndie atakuwa Nahodha mpya wa Man United baada kuondoka Nemanja Vidic mwishoni mwa Msimu huu kufuatia kumalizika Mkataba wake.

Wakati huo huo, Man United inatarajiwa kwenda Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu mara baada ya Mechi yao na Arsenal hapo Jumatano Usiku kwa Ziara ya Mazoezi.
Baada ya Mechi hiyo na Arsenal, Man united hawana Mechi nyingine hadi baada ya Siku 10 watapoivaa Crystal Palace.

No comments:

Post a Comment