|
Simba |
|
Mbeya City |
Simba SC,
imeonja joto ya jiwe baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mgambo Shooting, mechi iliyopigwa jana katika
Uwanja wa Mkwakwani, mjini Tanga.
Bao hilo
la pekee liliwekwa kimiani na Maganga Fully, dakika ya 29, akimalizia kazi
nzuri kutoka kwa Peter Mwalyunzi, bao lilipokewa kwa hisia chungu mbele ya
mashabiki wa Simba, ikiwa ni mwendelezo wa Ligi ya Tanzania Bara inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.
Huko Tabora Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, wenyeji Rhino Rangers walishindwa kuutumia vema Uwanja wa nyumbani baada ya kufungwa na Coastal Union bao 1-0.
Mbeya City imesambaratisha Mtibwa kwa kuifunga mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Kwa matokeo hayo Azam inaendelea kuongoza ligi kifuatiwa na Yanga huku Mbeya City na Simba ipo nafasi ya nne
No comments:
Post a Comment