Arsene Wenger anaamini kuwa tishio kubwa kwao ni toka kwa Nahodha wake wa zamani Robin van Persie wakati Manchester United itakapotua Emirates Jumanne Usiku kucheza na Arsernal kwenye Mechi ya Ligi Kuu Endland.
Van Persie, aliihama Arsenal Agosti 2012, na kuisaidia Man United kutwaa Ubingwa wa England katika Msimu wake wa kwanza tu huko Old Trafford chini ya Meneja Sir Alex Ferguson lakini Msimu huu chini ya Meneja mpya David Moyes Mabingwa hao wanayumba vibaya.
Arsenal wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 55 wakati Man United wako Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 41.
MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:
Wenger, ambaye anataka Timu yake iibuke vyema baada ya kutandikwa 5-1 katika Mechi iliyopita ya Ligi huko Anfield walipoaibishwa na Liverpool, ametaja Robin van Persie ndie tishio kwao aliposema: “Van Persie ni Mchezaji bora. Ni juu yetu kujilinda dhidi yake. Nadhani kufungwa na Liverpool ni ajali na tutajibu na Man United!”
Katika Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliyochezwa huko old Trafford, Man United iliifunga Arsenal Bao 1-0 kwa Bao la Van Persie.Per Mertesacker na Yaya Sanog kwenye mazoezi ambapo Yaya Sanog anaweza kukipiga kesho wakati Arsenal watakapoikaribisha Man United Emirates.
Mechi hii itakuwa na Balaa lake, arsenal wanataka kurudisha Heshima yao baada ya kubondwa na Liverpool bao 5-1 huku United wakitaka kumbana tena Arsenal kileleni na huku wakiwa hawana raha baada ya mechi yao ya mwisho kutoka sare OLD Trafford juzi kwa kutoka 2-2.Ozil
Mchezaji Bacary Sagna akionesha mbwembwe zake wakati wa mazoezi kwenye
uwanja wa London Colney kwa mara ya mwisho kabla ya kukutana na
Manchester United kesho jumatano kwenye kipute cha Ligi kuu England.
Lukas Podolski mbele akifurahia jambo na wenzie Tomas Rosicky pamoja
na Santi Cazorla (katikati) kwenye uwanja wa London Colney.
Mikel Arteta
Bosi Arsene Wenger akitoa maelekezo kwa Jack Wilshere mapema kwenye mazoezi kabla ya kukutana na United kwenye uwanja wao Emirates
Mastraika: Podolski na Alex Oxlade-Chamberlain
No comments:
Post a Comment