Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 11, 2014

COPA DEL REY: MARUDIANO - ATLETICO DE MADRID vs REAL MADRID, REAL SOCIEDAD vs FC BARCELONA KUCHEZWA LEO

Klabu za Real Madrid na Barcelona, wana nafasi kubwa leo Usiku kufuzu kutinga Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey, wakati wakicheza Mechi za Marudiano ya Nusu Fainali huku wote wakiwa na ushindi mnono toka Mechi zao za kwanza.

Real Madrid wataingia huko Estadio Vicente Calderon kucheza El Derbi madrileño na Watani zao wa Jadi, Atletico Madrid, huku wao wakiwa mbele kwa Bao 3-0.
Nao Barcelona watarudiana Estadio Anoeta na Real Sociedad ambayo waliifunga Bao 2-0 katika Mechi ya kwanza.

Baada kupigwa 3-0 na Real Madrid huko Santiago Bernabeu Wiki iliyopita, Atletico Madrid, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey, Wikiendi hii walifungwa na Almeria kwenye Mechi ya La Liga na kupokonywa uongozi wao wa Ligi hiyo.
Licha ya kuwa ni El Derbi madrileño, Atletico wana nia ya kulipa kisasi kwa Real na pia kujitayarisha wakati Timu hizi zitakapocheza Dabi nyingine hapo Machi Mosi na safari hii ikiwa ni Mechi ya La Liga.

Wakati Real itamtumia Cristiano Ronaldo ambae yuko kwenye Kifungo cha Mechi 3 kwenye Mechi za La Liga tu na Juzi kuikosa Mechi ya kwanza Real walipoifunga Villareal 4-2, Atletico watakuwa na upungufu mkubwa kwa kuwakosa Majeruhi Tiago, David Villa na Filipe Luis.
Kwa Barcelona, faraja kubwa ni kumwona Supastaa wao Lionel Messi akianza tena kucheka na nyavu apendavyo baada Jumapili kupiga Bao 2 wakati Barcelona inaichapa Sevilla 4-1 kwenye La Liga.RATIBA:COPA DEL REY
NUSU FAINALI
Marudiano
Jumanne Februari 11

23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [0-3] [Estadio Vicente Calderon]
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2] [Estadio Anoeta]

FAINALI
Aprili 19

No comments:

Post a Comment