BENDI ya Extra Bongo, ‘Wazee wa kizigo’
imewasimamisha wanamuziki wake wawili kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Wanamuziki
waliosimamishwa ni rapa Frank Kabatano na mwimbaji Redo Mauzo
baada ya kwenda Mbeya kujiunga na TOT
Plus kwa ajili ya sherehe za CCM kutimiza miaka 37 bila ruhusa ya uongozi wa
Extra Bongo.
Akizungumza jijini, msemaji wa bendi hiyo Juma Masesa alisema kuwa wanamuziki hao wamesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa kosa la utovu wa nidhamu kwani walikwenda Mbeya bila ya ruhusa ya uongozi.
“Wana muziki Frank Kabatano ambaye ni
rapa na Redo Mauzo ambaye ni mwimbaji
wamesimamishwa kwa utovu wa nidhamu kwani waliondoka kwenda Mbeya kufanya shoo
na bendi ya TOT Plus bila uongozi kuwa na taarifa”, alisema Masesa.
Kwa sasa Ally Choki "Mzee wa
Farasi" anarapu mwenyewe kwenye shoo za Extra Bongo japo rapa Ngosha
Masanja ambaye alipata kuwa na bendi ya Tamarin
Band, Vibration Sound na Mashujaa Band yupo kwenye majaribio na bendi hiyo
Extra Bongo
itakuwa haina mwanamuziki yoyote Mcongo baada ya kuachana na Papii Catalogue
mkataba wake ulipomalizika.
Kabatano ana
sifa ya kumudu vizuri rapu ya bendi hususan baada ya Extra Bongo kuachana na
Grayson Semsekwa aliyekwenda Twanga Pepeta na Saulo Fergusson aliyehamia Mashujaa
Band.
No comments:
Post a Comment