Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 11, 2013

VYAKULA VYA ASILI KEM KEM TAMASHA LA HANDENI

Na Mwandishi Wetu, Handeni
BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani. DC ni miongoni mwa viongozi wa juu serikalini wanaoliunga mkono Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza wilayani Handeni, huku likisubiriwa kwa hamu na wadau wa utamaduni na maendeleo hapa nchini.
Kambi Mbwana, Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni, maarufu kama Handeni Kwetu 2013, pichani. Maandalizi yamezidi kupamba moto na watu wote wanakaribishwa kujionea burudani za aina yake kwenye tukio hili la aina yake.
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.
Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo Desemba 9 mwaka huu.
“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyakula vya asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.
“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa 2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan wapenzi wa utamaduni hapa nchini.
 
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara,  Abdallah Kigoda

No comments:

Post a Comment