Timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la
Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es
Salaam leo.
Kilimanjaro
Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa
ndege ya RwandAir.
Wenyeji
Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada
ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana
Uwanja wa Nyayo.
No comments:
Post a Comment