Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limepata wajumbe
wapya wa wanne wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi uliofanyika leo hoteli ya Hillpark jijini Nairobi.
Uchaguzi
huo ulifuatiwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA ulioongozwa na Mwenyekiti wake
Leodegar Tenga na kuhudhuriwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kalusha Bwalya na ofisa wa Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA), Emmanuel Maradas.
Rais
wa zamani wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence
Mulindwa ndiye aliyeongoza katika uchaguzi huo ambapo wasimamizi walikuwa
Bwalya na Maradas.
Mulindwa
alipata kura zote 12 na kufuatiwa na Tariq Atta wa Sudan (10), Abdigaani Saeb
Arab wa Somalia (9) na Raoul Gisanura wa Rwanda (8). Atta, Arab na Gisanura
walikuwa wakitetea nafasi zao.
Walioshindwa
ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Sudan Kusini (SSFA), Alei Chabor aliyepata
kura tano na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya
aliyepata kura nne.
No comments:
Post a Comment