NEWCASTLE YAIFUNGA CHELSEA 2-0, MOURINHO AKWAMIA ST. JAMES PARK, ANUNA NA KUPEWA KICHAPO CHA AIBU
Chelsea leo ikicheza Ugenini imenyukwa bao mbili na timu ya Newcastle walipocheza leo kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mabao ya Newcastle yote yamefungwa kipindi cha pili katika dakika 68 kupitia mchezaji Yoan Gouffran baada ya kupigwa frii kiki na Yoan kujitisha kichwa safi na kufunga bao hilo mbele ya mabeki wa Chelsea. Bao la pili ni la jitihada baada ya Loïc Remy kufunga bao hilo dakika za majeruhi dakika ya 89 kwa kupewa pasi safi na kuachia shuti lililogonga mwamba na kuishilia kwenye lango la Chelsea.
Post a Comment