Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 13, 2013

BEKI WA MAN UNITED NEMANJA VIDIC ATOKA HOSPITALINI.

Nahodha wa timu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Nemanja Vidicameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata majeraha wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Arsenal.

Vidic alilazimika kutoendelea na mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao klabu ya Arsenal baada ya kugongana na mlinda mlango wake, Daivid De Gea wakati wakijaribu kuokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni mwao. 

Mara baada ya kuanguka Vidic aliweza kusimama tena lakini akashindwa kuendelea na mchezo na kukimbizwa hospitali kwa uchunguzi zaidi baada ya kuchukua muda uwanjani wakati madaktari wa timu wakimkagua. 
Kwenye taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo wawww.manutd.com, imesema kuwa Nemanja Vidic ameruhusiwa kutoka hospitali na sasa atakuwa nje ya uwanja kwa angalau wiki moja zaidi na anatarajiwa kurejea tarehe 24 ya mwezi huu wakati timu yake itakapocheza na Cardiff.
Taarifa hiyo imesema kuwa Vidic aliumia sehemu ya taya na sehemu ya kichwa kutokana na kujigonga kwa nguvu na mlinda mlango wake. 

Hivi karibuni mlinda mlango wa Tottenham, Hugo Lloris aligongwa sehemu ya kichwa na madaktari wake kumruhusu aendelee na mchezo jambo ambalo lilikosolewa vikali na wataalamu wa soka wakihofia afya yake. 
Kwenye mchezo wa Man utd na Arsenal, Man utd ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment