Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

TBL YAMWAGA MAMILIONI FAINALI ZA POOLTABLE TAIFA



KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari  imetangaza zawadi za washindi wa mashindano ya mchezo wa pool table kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Morogoro kuanzia Agosti 19-23 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari, Oscar Shelukindo alisema kuwa bingwa atapata 5,000,000, kikombe na medali za dhahabu, mshindi wa pili 3,500,000, kombe na medali za fedha na mshindi wa tatu atapata 1,250,000, kombe na medali za shaba.

Pia kutakuwepo zawadi za washindi mmoja mmoja ambapo kwa upande wa wanaume bingwa atapata 500,000, kikombe na medali ya dhahabu huku wanawake bingwa akipata 350,000, kikombe na medali ya dhahabu, mshindi wa pili kwa wanaume atapata 250,000 na medali ya fedha wakati kwa upande wa wanawake atapata 200,000 na medali ya fedha huku mshindi wa tatu kwa wanaume atapewa 200,000 na medali ya shaba na wanawake atapata 150,000 na medali ya shaba.

Wachezaji bora toka ngazi ya mkoa hadi taifa watapata ngao kila mmoja na medali ya dhahabu.
Naye Katibu mkuu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga alivitaja vilabu vitakavyochuana mjini Morogoro ni Bus stand ya Lindi, Balele ya Kagera, Loriondo ya Tabora, Paseansi ya Mwanza, King Palace ya SDhinyanga, Ngarenaro ya Arusha na Mbosho ya Kilimanjaro

Nyingine ni wenyeji Anatory ya Morogoro, Spider ya Tanga, Supersport ya Manyara, Yakwetu ya Pwani, Mpo Afriksa ya Temeke, Mashujaa ya Ilala, Topland ya Kinondoni, Atlantic ya Dododma, Garden ya Iringa na Royal Zambezi ya Mbeya.

Kafwinga aliviasa vilabu kuendeleza nidhamu walionyesha tangu ngazi za awali ili kuendelea kuupa heshima mchezo huo.

No comments:

Post a Comment