Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

BLATTER KUPELEKA OMBI KAMATI YA UTENDAJI KUBADILI KALENDA YA KOMBE LA DUNIA 2022.


Hatimaye Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekuabli kuwa itakuwa ni kosa kuipa nafasi Qatar ya kuandaa fainali ya kombe la dunia 2022, baada ya kufahamu kuwa fainali ya kombe la dunia kuandaliwa katika kipindin cha majira ya kiangazi kuwa italeta shida kubwa.
Taifa hilo la Kiarabu lilipewa nafasi ya kuandaa fainali ya mwaka 2010 lakini kulikuwepo
na malalamiko yaliyotolewa kuhusu usalama wa wachezaji katika kufanya tukio hilo katika miezi ya majira ya joto ambapo joto inaweza kufikia nyuzi 50.
 
Mwezi Februari 2011, alisisitiza kuwa kombe la dunia 2022 litafanyika katika kipindi cha kiangazi lakini sasa amebadili moyo wake na mwezi ujao anatarajiwa kupeleka ombi katika kamati ya utendaji ya FIFA kubadili tarehe ya tukio hilo na kuelekea majira ya baridi.

Blatter ameongea na told insideworldfootball akisema 

"Baada ya majadiliano na kufanya mapitio juu ya suala zima, nimekuja na hitimisho kuwa kucheza kombe la dunia katika joto la kiangazi huko Qatar si jambo la busara licha ya ukweli kwamba ina namna ya kutumia technolojia ya kupoza hali ya hewa.

Blatter amesema kuwa hilo litakubaliwa na kamati yake ya utendaji.

No comments:

Post a Comment