Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 11, 2013

ROONEY ATANGAZA BIFU RASMI NA MOYES

 
MSHAMBULIAJI  Wayne Rooney ametangaza ‘bifu’ rasmi na kocha wake mpya, David Moyes, baada ya kutumia mtandao wake wa kijamii wa Facebook kumtosa, huku akimshukuru kocha wa timu ya Taifa ya England, Roy  Hodgson, kwa imani na msaada anaoonesha kwake.

Uhasama kati ya  Rooney na kocha huyo wa Manchester United umeongezeka usiku wa kuamkia jana, baada ya mshambuliaji huyo aliyekosa furaha  kutumia ukurasa huo wa Facebook kutuma ujumbe akimshukuru Hodgson bila kumzungumzia Moyes.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, katika ujumbe huo mshambuliaji huyo alitoa salamu nyingi kwa Hodgson bila kutuma shukrani hata moja kwa kocha huyo Old Trafford. “Shukrani nyingi kwako Roy Hodgson,” ulieleza ujumbe huo ambao unatafsiriwa ni shukrani za kuungwa mkono na kocha huyo wa timu ya Taifa ya England katika tatizo la kukwama uhamisho wake kwenye klabu hiyo ya  Old Trafford.

Katika ujumbe huo pia Rooney alimshukuru Hodgson kwa kumchagua kwenye kikosi cha England ambacho Jumatano kitaivaa Scotland kwenye mechi ya kirafiki, lakini akashindwa kabisa kumgusia kocha wa klabu kupitia ujumbe huo wa mtandao wa kijamii.

Mshambuliaji huyo, ambaye yupo njia panda kuhusu ofa ya pauni milioni 30 iliyotangazwa na Kocha wa Chelsea,  Jose Mourinho, anaonekana kuchanganyikiwa zaidi siku za hivi karibuni, baada ya kuonesha wazi mawazo yake ya kutaka kuondoka.

.Akitoa shukrani zake zaidi kwa kocha huyo, alisema: “Siwezi kusubiri kujiunga na kikosi cha  England  na nina matumaini nitacheza kwa kushinda kama ilivyo mara zote dhidi ya  Scotland.
“Shukrani nyingi zimwendee  Roy Hodgson kwa kunichagua na kuonesha imani na msaada kwangu,  nalitambua hilo,” aliongeza nyota huyo.

Kauli hiyo imekuja siku ambayo  Rooney ameanza mazoezi na kikosi cha England kwenye Uwanja wa  Carrington na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21, kikiongozwa na Nicky Butt, huku akihitaji muda wa wiki nyingine moja ili aweze  kucheza kikosi cha kwanza.


No comments:

Post a Comment