Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 11, 2013

MAMBO 9 USIYOFAHAMU KWA RONALDO


MADRID, Hispania
MCHEZAJI Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya wachezaji wenye majina katika kizazi  hiki.

Mbali na kuwa na jina, nyota huyo anaonekana kuwa kwa sasa ni mchezaji bora wa dunia, akichuana na kinara mwingine, Lione Messi  kwa sasa.
Umahiri wake wa kutandaza kandanda ndiyo ulimfanya atwae taji la mchezaji bora wa mwaka 2008, linalotolewa  na Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA iitwayo  Ballon d'Or na ameshafunga mabao 201 katika mechi 199 alizoichezea  Real Madrid.
Hata hivyo, pamoja na umaarufu huo, kuna mambo mengine tisa usiyoyafahamu kuhusu kinara huyo.

1. Jina lake kamili:  Ronaldo dos Santos Aveiro
Alipewa jina hilo akirithishwa la Rais wa zamani nchini Marekani, Ronald Reagan, kiongozi ambaye alikuwa akipendwa  na baba yake.

2. Tabia yake: Mjeuri
Inasemekana Ronaldo ni mjeuri muda wote na kwamba wakati akiwa mdogo aliwahi kumpiga mwalimu wake na  kiti chake baada ya kudharau kazi yake ya darasani.

3. Kujiamini:
Cristiano Ronaldo mara zote huwa akikaririwa akijinadi kuwa yeye ni bora.
Inadaiwa kuwa tabia hiyo amekuwa nayo tangu azaliwe akijiita yeye kuwa ni bora bila wasiwasi wowote.
Kocha wake wa Sporting Lisbon anasema kwamba wakati akichezea timu hiyo alikuwa akijaribu kupangua mabeki wawili hadi watatu ili kudhihirisha uwezo wake.

4. Mitindo:
Cristiano Ronaldo amekuwa akijishughulisha na masuala ya mitindo ya nguo ambapo hadi sasa ana maduka mawili nchini Ureno aliyoyapa jina la CR7.
Maduka hayo kwa sasa yanasimamiwa na dada zake wawili  na huku yeye binafsi akionekana mwenye kupenda kuvaa nguo za mitindo.

5. Upasuaji:
Cristiano Ronaldo aliwahi kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati akiwa ana umri wa miaka 15.
Alifanyiwa upasuaji huo, baada ya madaktari kusema kuwa  ilikuwa ni lazima kutokana na kwamba matatizo aliyokuwa nayo yangeweza kuharibu kazi yake.

6. Hawezi kuvumilia timu yake ikifungwa
Inasemekana  Ronaldo alipokuwa mdogo alikuwa akiangua kilio wakati wenzake walipokuwa wakishindwa kufunga mabao, baada ya kuwatengenezea mipira, jambo ambalo lilisababisha apachikwe jina “Mtoto wa kulialia”.
Katika mahojiano mwaka  2011, aliwahi kusema wanapokuwa kwenye bwawa la kuogelea yeye na rafiki yake wa kike huwa wanashindana kuogelea na mwanzo huwa anamuacha atangulie kushinda lakini wanapokaribia mwisho huwa anajitahidi kumshinda kwa kile alichodai ni kwamba huwa hawezi kuvumilia kushindwa.

7. Bidhaa za matangazo:
Ronaldo anatangaza bidhaa za kampuni kubwa kama vile  Nike na  Armani Exchange.
Kipindi kilichopita aliweza kuweka rekodi ya kuingiza dola za ziada milioni 25 kwa kupitia biashara ya kutangaza bidhaa hizo.

8. Kujichora mwili:
Ronaldo hana tattoo yoyote kwenye ngozi ya mwili, jambo ambalo linamfanya aweze kuchangia damu mara mbili kwa mwaka. Mbali na hilo, nyota huyo hanywi pombe kwa sababu bado ana kumbukumbu ya ugonjwa uliomkumba baba yake kutokana na madhara ya pombe.

9. Liverpool walikuwa na bahati mbaya kwake
 Klabu ya soka ya England, Liverpool mwaka 2002 ilikuwa na nafasi ya kumnasa  Cristiano kwa kitita cha pauni milioni 12.2,  lakini wakashindwa kufanya hivyo kwa sababu waliona hana uwezo wa kutosha.

No comments:

Post a Comment