Simba Sports
Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia
makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafahamika kama “OCB”)
kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (strategic plan).
Mchakato huo
unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na makamu mkuu wa
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo
imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi
yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-
1. Kuhusu
makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na
maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
3. Kupitia
mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na
mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa
ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.
Katika kikao
cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013 Referal Committee ya Simba Sports Club
iliyochaguliwa ni:-
1. Joseph
Itang’are
2. Swedy
Mkwabi
3. Francis
Waya
4. Ramesh
Patel
5. Evance
Aveva
6. Mulamu
Ng’hambi
7. Salim
Mhene
8. Mtemi
Ramadhani
9. Moses
Basena
10. Henry
Tandau
11. Omary
Gumbo
12. Michael
Wambura
13. Glory
Nghayomah
14.
Crensencius Magori
15. Honest
Njau
16. Ruge
Mtahaba
17. Evodius
Mtawala
18. Dr
Mwafyenga
Kikao cha
kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
Uongozi wa
Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu
ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi
(professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu
yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya
klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili
kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani
ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand
goodwill) ili kuvutia wawekezaji.
Mpango
mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa
utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta
kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa
wadau na wanachama wa klabu.
Mpango
mkakati huo utakuwa tiyari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu
wa mwaka 2013/2014.
Imetolewa na
Evodius
Mtawala
Katibu Mkuu,
Simba Sports
Club.
9/5/2013
No comments:
Post a Comment