Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 4, 2013

VIPI MESSI PALE BARCA, GOTZE ATAFITI NAFASI GANI BAYERN?



BERLIN, Ujerumani
MATANGAZO mawili yaliushitua umma wa mchezo wa soka kwa mwaka huu wa 2013. Tangazo la kwanza ni kuhusu Pep Guardiola kwamba atachukua mikoba ya kuinoa Bayern Munich mwisho wa msimu huu - huku kocha huyo wa zamani wa Barcelona akikataa ofa tamu kutoka England na badala yake kukubali kujiunga na mikikimikiki ya Bundesliga.
Tangazo la pili ni la uhamisho wa kushitukiza wa Mario Gotze, kijana mwenye kipaji cha kipekee kwenye soka na kumfanya Wajerumani wampachike jina la 'Lionel Messi wa Ujerumani', ambaye ataihama Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu na kutua Allianz Arena.
Kocha wa BVB, Jurgen Klopp alithibitisha kwamba staa huyo wa Nationalelf atahamia Allianz Arena msimu ujao kwenda kufanya kazi sambamba na Guardiola, jambo ambalo kwa sasa limeibua mjadala juu ya Mhispania huyo atamtumia wapi Gotze kwenye kikosi hicho cha Bayern.

AKICHEZA KAMA No.9 BANDIA
Mfumo: (4-2-3-1/4-3-3)
Kikosi: Neuer, Lahm, Dante, Badstuber, Alaba, Martinez, Schweinsteiger,
Muller, Kroos, Ribery, Gotze.
Kitu maarufu zaidi alichowahi kukifanya Guardiola katika kikosi cha Barcelona ni kuweza kumhamisha Messi kutoka wingi ya kulia na kucheza kama mshambuliaji wa kati.
Katika zama zake ndani ya Nou Camp, washambuliaji halisi walikuwa hawana nafasi kwake na jambo hilo ndilo lililowafanya Samuel Eto'o na Zlatan Ibrahimovic kuondoka, huku Thierry Henry akiwekwa kando baada ya timu hiyo kuwa chini yake na kumpa nafasi Pedro.
Kwa kuwalinganisha Messi na Gotze wamekuwa wakicheza nafasi zinazofanana, hasa ukizingatia kwenye kikosi chake cha BVB na hata kwenye mechi ya timu ya taifa ya Ujerumani ilipocheza dhidi ya Kazakhstan, Gotze alitumika kama mshambuliaji wa kati bandia.
Kama mpango wa Guardiola utakwenda sawa, basi mshambuliaji Mario Gomez hatakuwa na chake tena ndani ya Allianz Arena, huku wachezaji kama Mario Mandzukic na Claudio Pizarro watakuwa mpango mbadala kama mambo hayatakwenda sawa katika mfumo wake wa kumtumia Gotze kama mshambuliaji wa kati.

KUMPOKA NAMBA KROOS
Mfumo: (4-2-3-1)
Kikosi: Neuer, Lahm, Dante, Badstuber, Alaba, Martinez, Schweinsteiger,
Muller, Gotze, Ribery, Mandzukic.
Ukweli ni kwamba soka la Hispania na Ujerumani ligi zake zipo tofauti sana. Washambuliaji kwenye Bundesliga siku zote wamekuwa ni wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mipira na kuwachezesha viungo wa kati.
Guardiola atakua amelifahamu hilo vizuri kwa kipindi ambacho amekuwa na Bayern hadi sasa, lakini hilo halina maana kwamba mshambuliaji Mario Mandzukic atakuwa na uhakika wa kupata namba katika kikosi cha kwanza.
Lakini, itakuwa jambo la hatari sana kumwondoa Mcroatia huyo kwenye kikosi hasa ukizingatia amefanya mambo mengi yaliyowaduwaza mashabiki wa Bayern tangu alipojiunga mahali hapo akitokea Wolfsburg mwaka jana na kwasasa ni kinara wa mabao akiwa amechunga mara 21 katika michuano yote.
Wakati Toni Kroos akifurahia kiwango chake bora, Mjerumani huyo alishindwa kuonyesha mahali tangu duru la pili lilipoanza kutokana na kupata majeruha ambayo yalimweka nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu ilipoanza Aprili.
Kama Pep atadhani kwamba Kroos bado hajarudi kwenye kiwango chake cha ubora, basi kwenye nafasi hiyo anaweza kumtumia Gotze badala yake na kukifanya kikosi hicho kuwa na uwiano hatari zaidi katika soka la Ulaya na Bundesliga.

KAMA MRITHI WA RIBERY
Mfumo: (4-2-3-1/4-3-3)
Kikosi: Neuer, Lahm, Dante, Badstuber, Alaba, Martinez, Schweinsteiger,
Muller, Kroos, Gotze, Mandzukic.
Katika kipindi chake bora kabisa kwenye kikosi cha Borussia Dortmund, Gotze amekuwa hatari zaidi alipokuwa akicheza nyuma ya Robert Lewandowski, kitu ambacho kinakufanya usiamini kuwa staa huyo pia ni hatari anapocheza kama winga, mahali ambapo amelifanya jina lake kutambulika.
Kutokana na kuwa na kasi, uwezo mkubwa wa kukokota mpira na ufundi wa ziada, Gotze anaonekana kuwa hana tatizo kwenye kucheza wingi na kutazamwa kama mrithi wa Franck Ribery, ambaye kwa sasa ameshaanza kuwa na umri mkubwa.
Gotze, wakati alipocheza kushoto kwenye mechi dhidi ya Real Madrid ilionekana wazi kuwa na uwezo, wakati alipopiga krosi kwa Lewandowski, aliyefunga bao la kwanza katika ushindi wao wa 4-1.
Na kutokana na uwezo wa kushambulia wa beki wa pembeni David Alaba, jambo hilo litamfanya Gotze aingie katikati ya uwanja ambapo pamoja na Kroos na Thomas Muller, wataweza kuunda safu ya viungo washambuliaji watatu - ambao kila mmoja hatari iliyopo ni kwamba ana uwezo wa kufunga.
Lakini, Ribery amekuwa kwenye msimu bora kabisa hivyo, suala la kumbadili Mfaransa huyo litakuwa mtihani mgumu sana kwa Pep.

KUCHEZA UPANDE WA KULIA
Mfumo: (4-2-3-1/4-3-3)
Kikosi: Neuer, Lahm, Dante, Badstuber, Alaba, Martinez, Schweinsteiger,
Gotze, Kroos, Ribery, Mandzukic.
Wakati Thomas Muller akifurahia msimu bora kabisa katika maisha yake ya soka hadi kufika sasa, akifunga mabao 20 na kutengeneza mengine yasiyohesabika, si sahihi kusema kwamba si mchezaji wa kiwango cha Guardiola.
Utendaji wake wa kazi ndani ya uwanja, kujitolea na moyo wa kutoogopa, umemfanya kuwa mchezaji muhimu kabisa katika kikosi ch Bayern na hakika hata kama angekuwa kwenye kikosi cha Barca zama zile za Guardiola, basi nyota huyo angepata namba tu.
Gotze, uwezo wake wa kucheza kulia uliipa faida Dortmund hadi hapo Shinji Kagawa alipoondoka ambapo Jurgen Klopp aliamua kumwingiza kati na kutokana na Philipp Lahm, Kroos na Bastian Schweinsteiger kucheza namba zinazofanana kama katika timu yao ya taifa, Guardiola anaweza akahitaji kumtumia Gotze katika namba yake ya asili, upande wa kulia.
Muller, kwa upande wake ni mchezaji ambaye mkataba wake utakomea 2017 na hivyo mara kadha amekuwa akizungumzia matakwa yake ya kutaka kuwa gwiji la Bayern, jambo ambalo litakaloweza upinzani mkubwa wa namba kwenye kikosi hicho kama Gotze atakuwa anatumika kwenye upande wa kulia, nafasi ambayo anacheza staa huyo wa Ujerumani, Muller.

No comments:

Post a Comment