LONDON, England
ARSENE Wenger ameonyesha nia ya kuendelea kubaki Arsenal, licha
ya kuhusishwa na taarifa za kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain.
Wenger alieleza nia yake ya dhati ya kuendelea kubaki Emirates,
katika kipindi hiki ambacho Arsenal wanapambana kumaliza miongoni mwa timu nne
za juu kweli Ligi Kuu England.
“Nataka kubaki kama nikifanya vizuri, kama klabu ikiona
nimefanya vizuri,” Wenger aliwaambia waandishi wa habari.
“Nataka klabu hii ifanye vizuri. Timepitia kipindi kigumu,
lakini naamini klabu iko kwenye nafasi nzuri ya kufanya vuzuri siku zaa usoni,
“Nafanya kazi yangu kwa kujitoa kwa kila kitu, na ni mtiifu
kwao. Najaribu kufanya vizuri kadri niwezavyo kwa ajili ya hii klabu.”
No comments:
Post a Comment