Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angela Kairuki (Katikati) akiwa ameinua juu albam alizozindua jana kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza |
Kapotive kwaya wakitumbuiza |
Kapotive |
Upendo Nkone pia alikuwepo |
Masanja Mkandamizaji pia alikuwepo |
NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki amesema
serikali ipo pamoja na wasanii katikati kulinda haki za kazi zao.
Angela aliyasema hayo juzi wakati akizindua albamu mbili za
kikundi cha kwaya ya Kapotive toka Kagera iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo
Plaza jijini Dar es Salaam.
“Nawapongeza Kapotive kwa kazi zao nzuri kwani kimekuwa
kikundi cha mfano kinachotoa huduma ya kiroho kupitia nyimbo, kwani pia
kinaburudisha”, alisema Angela.
Pia naibu Waziri aliwachangia wanakikundi hao milioni moja
kwa ajili ya kuanzisha studio itakayokuwa inatengeneza kazi za wasanii
mbalimbali huko Kagera.
Kapotive ilizindua albamu mbili, moja ikiitwa Namshukuru
Mungu yenye nyimbo 10 na nyingine Yesu ni mwema yenye nyimbo nane.
Katika uzinduzi huo kwaya mbalimbali na zilitumbuiza akiwemo
Upendo Nkone na Emanuel Masanja maarufu kama Masanja Mkandamizaji aliyetumbuiza
wimbo wake uitwao ‘nipo busy’ na kuwafanya waliojumuika kusimama na kuimba na
kucheza pamoja naye.
No comments:
Post a Comment