Nyoshi El Sadat Rais wa FM Academia akionyesha manjojo yake kwa waandishi wa habari leo |
Lilian Internet akionyeshastaili ya kibega na mgongo |
Anti Suzy pia alionyesha manjonjo yake |
WAPENZI wa
muziki wa dansi katika jiji la Dar es Salaam Jumamosi hii watapata burudani ya
aina yake wakati bendi mbili maarufu za muziki huo za FM Academia na Mashujaa, zitakapopanda
jukwaa moja katika onyesho maalum za uzinduzi wa mauzo ya albamu Risasi Kidole
ya bendi ya Mashujaa.
Onyesho hilo
la pamoja litafanyika kwenye ukumbi wa Business Park uliopo Kijitonyama jijini
Dar es Salaam ambapo bendi hizo zimekubaliana kufanya ushirikiano maalum ambao
utakuwa ni muendelezo wa ushirikiano wa kufanya maonyesho ya pamoja kwa bendi
za muziki wa aina hiyo hapa nchini.
Wakizungumza
na waandishi wa habari leo, viongozi wa bendi hizo wamesema kuwa onyesho hilo
litakuwa la aina yake ambapo pamoja na burudani bendi ya Mashujaa itakuwa
ikizindua rasmi uuzaji wa albamu yake hiyo ambayo ni ya kwanza.
“Albamu yetu
ina jumla ya nyimbo tisa, onyesho hili ni maalum kabisa kwa ajili ya kuzindua
mauzo ya alabu yetu, katika hili tumeona tuanze pia ushirikiano wa kufanya maonyesho
ya pamoja bendi zingine na sasa tunaanza kushirikiana na FM Academia,” alisema
Charles Baba, kiongozi wa bendi ya Mshujaa.
Kwa upande
wake Rais wa FM Academia, Nyoshi Al-Saadat alisema umefika wakati sasa bendi
ziwe na ushirikiano wa kweli, kwa lengo la kuinua muziki huo, na si kufanya
mashindano ambayo mwisho wake umekuwa ni kuvurugana.
Viongozi hao
waliwataka mashabiki wa muziki kufika kwa wingi katika Ukumbi wa Business Park
kushuhudia onyesho hilo ambalo litakuwa la aina yake kwa kuwa kila bendi imejiandaa vyema kwa
ajili ya kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.
No comments:
Post a Comment