Mkufunzi wa mchezo wa mpira wa kikapu kutoka Marekani Albert Sokaitis amewasili jijini Dar es Salaam baada ya kualikwa na Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania .
Katibu mkuu wa msaidizi wa shirikisho hilo Michael Maluwe amesema mkufunzi huyo atasaini kandarasi yake wiki hii lakini akuweka wazi kuwa itakuwa wa muda gani .
Maluwe amesema kuwa mkufunzi huyo atakaa kwa muda mrefu zaidi ili kuusaidia mchezo katika mafunzo mbalimbali ya makocha na wachezaji ili aweze kuuinua mchezo huo Nchini .
Maluwe ameongeza kwa kusema mengi kuhusu kandarasi na kazi atakazo fanya ni kuandaa timu tatu za umri tofauti na kuendesha semina na mafunzo kwa walimu wa mpira wa kikapu nchini .
Maluwe ameaongeza kwa kusema ujio wa mkufunzi huyo ni muhimu sana kwa kuukuza mchezo wa mpira wa kikapu .Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho la mpira wa kikapu kuleta mkufunzi wa muda mrefu ili kuleta changamoto za mpira wa kikapu . Maluwe " TBF inatazama zaidi kuendeleza mpira wa kikapu hasa kwa vijana na mashuleni ili kupata vijana zaidi waweze kuucheza mchezo huo .
No comments:
Post a Comment