Aneth Kushaba ameteuliwa kushindanishwa kwenye tuzo za Kili Music Award kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Bendi.
Msanii huyu ili aweze kushinda kwenye nafasi hiyo anahitaji sapoti yako katika kumpigia kura.
Ili kuweza kumpigia kura Andika sms Am 1 kwenda 15345 au www.kilitimetz.com kadri uwezavyo
Aneth ni mwuimbaji na meneja wa Bendi ya Skylight inayotoa burudani kwenye Ukumbi wa Thai Village Masaki kila mwishoni mwa wiki, pia alishawahi kushiriki kwenye Tusker project fame na kuwakilisha Tanzania vizuri.
Mwanadada huyu alishawahi fanya kazi kwenye B. band akiwa muimbaji na sasa anawapagawisha mashabiki akiwa na Skylight band
No comments:
Post a Comment