Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 26, 2013

WAREMBO 16 NJE SHINDANO LA MISS TABATA 2013




Jumla ya warembo 16 wametemwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Tabata ambao utafanyika Mei 31 Dar West Park.
Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana kuwa warembo hao wametemwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, kukosa sifa za kushiriki na utovu wa nidhamu.
Kalinga aliwataja warembo waliyotemwa kuwa ni Sophia Claud (21), Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Ray Issa (22), Shamim Abass (22), Shan Abass (22), Amina Ally (18), Magdalena Bhoke (21) na Zilpha Christopher (19)
Kalinga aliwataja warembo wanoendelea na mazoezi katika umbumbi wa Dar West Park, Tabata kila siku kuwa ni Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20) and Glory Jigge (18).
Wengine ni Rachel Mushi (20), Caroline Sadiki (20), Kabula Juma Kibogoti (20), Blath Chambia (23), Suzzane Daniel Gingo (18), Upendo Lema (22), Pasilida Mandari (21) na Martha Gewe (19).
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu. 
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Redds Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na chini ya Udhamini wa Redds, CXC Africa, Fredito Entertainment, Brake Points na Saluti5.

No comments:

Post a Comment