Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 24, 2013

SIMON MSUVA AMTIA HOFU LEIWING



Simon Msuva (katikati) akiwa na Haruna Niyonzima kulia na aliyepo kushoto ni Frank Domayo

WAKATI timu ya Simba ikibaki na matarajio ya kuwafunga watani wao wa jadi Yanga, ili iendeleze heshima baada ya kuukosa ubingwa, benchi la ufundi la timu hiyo limeelekeza mafunzo maalum kwa mabeki wa timu hiyo, ili kukabiliana na mashambulizi ya wapinzani hao hasa kumzuia kiungo wake hatari chipukizi Simon Msuva.

Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kinesi Ubungo jijini Dar es Salaam juzi na jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Liewig  alionekana kuwa makini zaidi na wachezaji wa safu ya ulinzi.

Akizungumza jijini kocha huyo, alisema amekuwa akikiandaa kikosi chake katika kila idara, lakini kwa sasa anaangalia zaidi sehemu ya ulinzi kutokana na umuhimu wa mechi zinazowakabili mbele yao.
Alisema, mechi yao ya kesho itakayowakutanisha na timu ya Ruvu Shooting, wanaipa nafasi kubwa kwa vile wanafahamu timu hiyo iliyopo kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa ligi, ina kiwango kizuri na imeonekana kuwa tishio kwenye michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Liewig alisema vilevile anaiandaa safu ya ulinzi kutokana na matayarisho ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga, itakayochezwa Mei 18 jijini Dar es Salaam.
Bila kutaja jina la mshambuliaji anayewapa kiwewe, kocha huyo alisema,  anaamini itakuwa ngumu kuliko zote kwa vile timu hiyo ina safu ya washambuliaji vijana na wenye kasi hivyo wanahitaji kuwa na mabeki imara.

Yanga hadi sasa inajivunia washambuliaji wake chipukizi akiwemo Frank Dumayo na Simon Msuva, hivyo tahadhari hiyo ya Liewig inaonyesha kuwahofia zaidi washambuliaji hao.
Hata hivyo Simba kesho inajitupa kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Ruvu Shooting ikiwa inawania pointi tatu ili iweze kuisogelea Kagera Sugar iliyopo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 40.

No comments:

Post a Comment