Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 15, 2013

RIDHIWAN KIKWETE AUNDA KAMATI YA KUMSAIDIA KUSIMAMIA UJENZI WA JENGO DOGO LA YANGA, WAPO VIGOGO WA BENKI KADHAA


Ridhiwani Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyeki wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam, ameteua Wajumbe wa kusaidia kazi hiyo wakiwemo wanasheria wawili na wataalamu wa Taasisi za Fedha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika uteuzi wa Kamati hiyo, amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Issa Hajji Ussi ambaye ni  Makamu wake na wajumbe ni Isaac Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, ambaye anafanya kazi  Beki ya Uwekezaji Tanzania (T.I.B.),  Alan Magoma,  ambaye ni Mwanasheria mkongwe, Mavale Msemo na Charles Palapala.

“Utaona kuna watu wengi wa taasisi za fedha ni kwa sababu zoezi hili linahitaji fedha hivyo tutaangalia kama tutaingia ubia na mtu, au sisi klabu tukawekeza kwenye mradi huo moja kwa moja,”alisema.
Kwa upande wa watendaji, Ridhiwan alisema kwamba Kamati yao itaongozwa na Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako, Beda Tindwa na Mahmoud Milandu.

“Kamati yetu sisi itakuwa ya kukaa na kutengeneza mipango na baadaye kama kutakuwa na barua ya kupeleka wapi, au mtu wa kufuatwa, basi ile kamati nyingine ndogo, itafanya kazi hiyo,”alisema.

No comments:

Post a Comment