Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000
kutokana na watazamaji 11,458. Viingilio katika mechi hiyo namba 155
iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
10,198,220.34. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45,
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh.
4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.
WATAZAMAJI
11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO
Watazamaji
11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na
Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na kuingiza sh. 63,170,000. Viingilio katika mechi hiyo namba 156
iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
9,636,101.69. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati
ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,762,250.29.
No comments:
Post a Comment