Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 23, 2013

MANCHESTER WAFANYA SHEREHE YA KUTWAA UBINGWA WA ENGLAND, KIBABU FERGUSON AJIMIMINIA SHAMPENI KWA RAHA ZAKE

Manchester United imetwaa rasmi ubingwa wa 20 wa taji la ligi kuu soka nchini England kwa ushindi wa mabao matatu ya aina yake dhidi ya Aston Villa,Mabao yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ambaye sasa atakuwa akiongoza safu ya wafungaji kwa kufikisha mabao 24 huku Luis Suarez akifuatia akiwa na mabao 23. 

Van Persie alifunga mabao yote matatu ndani ya dakika 31 za kipindi cha kwanza katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Traford na kuwafanya United kufikisha pointi tofauti ya 16 na waliokuwa mabingwa watetezi majirani zao Manchester City,huku wakiwa na michezo minne kibindoni.
Mkongwe Ryan Giggs alianza kwa kumtengenezea nafasi ya goli la kwanza Van Persie dakika mbili baada ya mchezo kuanza kabla ya Wayne Rooney kumpa nafasi nyingine nzuri Van Persie dakika ya 13 na kufunga moja kati ya mabao bora kabisa msimu huu kwa mguu wake wa kushoto na kufanya United kuwa mbele kwa mabao mawili ndani ya dakika 15 za kwanza za mchezo.
Alikuwa ni Giggs kwa mara nyingine aliyempa pande Van Persie na kufunga bao la tatu dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza na kufanya uwanja wa Old Traford kulipuka kwa shangwe za mashabiki,kwani ilikuwa dhahiri wamekwisha jihakikisha ubingwa msimu huu. 

Hii imekuwa mara ya nne kwa Manchester United kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Traford,baada ya kufanya hivyo mwaka 1999,2002 na 2009. Mara ya mwisho United kutwaa ubingwa wa ligi kuu huku wakiwa na michezo mingi iliyosalia ilikuwa mwaka 2001 baada ya kutangazwa mabingwa huku wakiwa na michezo mitano kibindoni.
Huu ni ubingwa wa 13 wa taji la ligi kuu ya Uingereza kwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo mwaka 1986.

Kwa matokeo hayo Aston Villa watasalia kwenye nafasi ya 17 wakiwa na pointi zaidi ya timu ambazo zipo kwenye hatihati ya kuteremka daraja. 

Manchester United wikiendi ijayo watapambana na Arsenal kwenye uwanja wa Emirates wakati wakisubiri kukabidhiwa kombe lao la ligi kuu katika mchezo wao mwisho kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Traford hapo May 12 watakapokuwa wakicheza na Swansea.
 Van Persie akionesha jezi yake, ambayo pia inawakilisha idadi ya vikombe vya Ligi Kuu vilivyobebwa na Man United.
 Shampeni ya Ushindi Hiyoooo!! Rio Ferdinand akitingisha na kuwamwagia wenzake shampeni ya kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu.
 Nina Furaha Kuliko Nyie Wote: Ferdinand akiruka juu kwa furaha wakati wa zoezi la kufungua shampeni ya kushangilia ubingwa.
 Hii Yangu Pekee: Ferguson akifungua shampeni yake ya kusherehekea ubingwa na kisha kuanza kuinywa kama anavyoonekana katika picha ya chini.

No comments:

Post a Comment