Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 13, 2013

CAF INAPOFANYA MABADILIKO YA SHERIA YA KUTATIZA INAFIKIRIA NINI?


Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limepitisha sheria ambayo mchezaji akifanya kosa katika mechi za kimataifa za klabu, kosa lake litaiathiri pia timu ya taifa lake kwani hataruhusiwa kucheza hadi amalize kutumikia adhabu husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema kuwa CAF wameagiza wanachama wake kuzingatia sheria hiyo ambayo itahusu makosa ya kinidhamu na makosa mengine yanayofanywa na mchezaji katika mechi za klabu za kimataifa.
 
“CAF wameagiza hivyo na hatuna namna kwa sababu sisi ni wanachama wake. Mchezaji akionyeshwa kadi nyekundu au kadi mbili za njano na kumlazimu akose mechi moja ama mbili, basi kama kuna mechi ya timu yake ya taifa itakayofuata maana yake ataikosa kwa sababu ya kutumikia adhabu hiyo,” alisema Osiah.
 
“Tunaomba wachezaji wawe na nidhamu ya hali ya juu katika mechi za klabu zao kwani mambo sasa ni magumu. Makosa ya mchezaji ndani ya klabu yataigharimu pia timu yake ya taifa,” alisema zaidi Osiah.
 
Katika siku za hivi karibuni, CAF wamekuwa wakiibuka na kanuni na sheria ambazo nyingine zimekuwa hazilingani kabisa na zile za mashirikisho mengine duniani.
 
 Kwa mfano, mwishoni mwa mwaka jana, CAF ilipitisha kipengele cha mgombea wa urais wa shirikisho hilo kuwakiwa atoke miongoni mwa wajumbe wa kamati yao ya utendaji, suala ambalo lilipitishwa kwa kura nyingi licha ya baadhi ya wajumbe, akiwamo Rais wa TFF, Leodgar Tenga kupinga vikali kifungu hicho.

No comments:

Post a Comment