Watazamaji
7,412 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Toto
Africans lililochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kuingiza sh. 42,508,000.
Mechi hiyo namba 135 iliyochezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 45 kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 9,406,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni
sh. 6,484,271.19.
Kiingilio cha
sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo
walikuwa 6,708 na kuingiza sh. 33,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki
ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 89 na kuingiza sh.
1,780,000.
Mgawo mwingine
wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,783,100.82, tiketi sh. 4,136,390,
gharama za mechi sh. 2,869,860.49, Kamati ya Ligi sh. 2,869,860.49, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,434,930.25 na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,116,056.86.
No comments:
Post a Comment