Bingwa
wa kickboxing, Hamis Mwakinyo, anatarajia
kupanda ulingoni kuzipiga na bingwa wa Taifa wa ngumi za kulipwa nchini
uzito wa light weight kg 60, Said mundi, wa Tanga katika pambano la raundi
nane.
SAIDI MUNDI KUSHOTI NA KING CLASS MAWE |
Hamis Mwakinyo ambaye ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa WKN-AFRIKA (World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa dunia nchini iran, atazichapa na mpinzani wake huyo, ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Aidha pambno hilo limezidi kuwa gumzo midomoni mwa mashabiki wengi wa mchezo huo, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa muandaaji wa pambano hilo Promota, Ally Mwanzoa, amesema kuwa mabondia hao tayari wameshakubaliana na kuridhia kutiliana saini mkataba wa makubaliano wa pambano hilo.
Mwanzoa, alisema kuwa pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa mabondia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania hususani jijini Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu za majaji wa mchezo huo kutoka nje ya Tanzania ili kuondoa malalamiko yeyote yanayoweza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment