Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda
akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa
Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha
kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.
Mwenyekiti wa Jukwaa la
wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu
Absalom Kibanda, amevamiwa usiku wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake
Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga
kichwani na kwenye jicho.
Kibanda ambaye amepata
majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo
alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
Matibabu lakini kuna uwezekano wa kupelekwa Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi
Taarifa hii imetushtua sana hasa sisi wafanyakazi wa New Habari kwani tulikuwa naye kazini hadi gazeti zinakwenda kwenye production. Tutaendelea kuwajuza zaidi
No comments:
Post a Comment